Load

Friday, November 9, 2018

JUA ZAO LA VANILA PAMOJA NA MATUMIZI YAKE

1.zao la vanila asili yake ni Amerika ya kati huko mexico,costa rica pamoja na guatemala ambako lilianza kutumika katika karne ya 15 na kufika ulaya katika karine ya 16.zao hili kwa sasa linazalishwa kwa wingi katika nchi za madagasca,comoro pamoja na reunion. Hapa nchi Tanzania zao hili lilianzishwa katika mkoa wa Kagera kutoka nchi ya jirani Uganda mnamo mwaka wa 1962 ,na pia katika mkoa wa Kagera ndimo kunako zalishwa zao hili kwa kiasi chake katika wiliya ya Muleba pamoja na Bukoba na pia huko Zanzibari.Pia zao hili limeweza kuleta fedha za kigeni katika nchi pamoja na kutoa ajira katika sehemu husika ambapo zao hili linazalishwa. MATUMIZI YA ZAO LA VANILA. *Zao hili hutumika kwa kuongeza ladha katika vyakula pamoja na katika vinywaji,Matumizi makubwa ya zao hili ni kuongeza harufu nzuri katika vyakula pamoja na vinywaji aina tofauti tofauti. *Vyakula hivyo ni pamoja na; 1;keki 2;maandazi 3;biskuti 4;chocolate 5;uji 6;barafu *vinywaji ni kama; 1;soda 2;juice Nb,pia zao la vanila hutumika pia katika kutengenezea vilainishi vya ngozi pamoja na manukato ya aina mbali mbali. 2.MAENEO YANAYO FAA KWA KILIMO CHA VANILA. Katika udogo wenye uwezo wa kupitisha maji,rutuba pamoja na mboji ya kutosha huweza kusitawisha vema zao hili la vanila,kivuli cha wastani maana zao hili alihitaji jua kali sana. 3;HALI YA HEWA INAYOWEZESHA ZAO LA VANILA KUSITAWI KWA UBORA. Zao hili la vanila linahitaji hali ya hewa lenye wastani wa joto la sentigredi 28,Lakini pia linaweza kustahimili katika hali ya joto la nyuzi 21 mpaka 30.Pia huitaji mvua zenye zenye mtawanyiko wa milimita kati ya 1,500 mpaka 3,000 pia katika milimita 2000 za mvua zao hili hustawi sana na kwa uzuri zaidi,kinahitajika zaidi kipindi cha kati ya miezi 2 hadi 4 cha ukavu ili kuwezesha mmea kuchanua maua. 4.TABIA YA MMEA WA VANILLA. Vanila ni zao ambalo hukua kwa kutambaa kwenye mti wa mhimili ,Pia huzalisha matunda yanayo fanania na maharagwe(ukubwa wake huwakati ya sentimita 10-25 cm).Mmea huu huweza kukua na kufikia urefu wa mita 10 hadi 15.Maua yake huwa makubwa ,manene na hunukia ,yana rangi ya kijani isiyo kolea pamoja na unjano. 5.UPANDAJI WA ZAO LA VANILLA. Miti ya jatropa pamoja na causarina katika mihimili yenye urefu wa sentimita 120 hadi 150.Baada ya kuikata iache ikauke vizuri kati ya siku 1 hadi 10.Kisha ipandwe pembeni mwa shimo kiasi cha sentimita 15 hadi 30. *Tayarisha marando yenye sentimita 90 (futi 3) mpaka sentimita 120 (futi 4),yaache yakauke kidogo kwa siku 7 hadi 10.Toa majani 3 toka sehemu ya chini ya rando .Marando marefu huanza kuchanua baada ya mwaka 1.5 hadi 2 bali marando mafupi huchelewa kuchanua ,huanzia miaka 3 hadi 4. *Panda marando hayo katika mashimo yaliyo tayarishwa katika kina cha sentimita 10 hadi 15 funika na gandamiza pia. 6.NAMNA YA KUHUDUMIA NA KULITUNZA SHAMBA LA VANILLA. Shamba liwe safi kila wakati. Kwa kutandaza nyasi kavu kwa ajili ya kuzuia uwepo wa magugu shambani pamoja na kutunza unyevunyevu ,Pia punguza mihimili kila inapofika urefu wa sentimita 180 ili kuwezesha uwepo wa kivuli kila yatokapo machipukizi lakini pia chavusha maua kila yanapo chanua kwa wakati .Muda wa kuchavusha huanzia saa 3 ahsubuhi hadi saa 7 mchana ,kifaa cha ncha kali kama pini,mwiba hutumika katika uchavushaji huo.Ua lililo chavushwa hukaa katika kikonyo ndani ya siku tatu wakati ua ambalo halijachavushwa kudondoka ndani ya siku moja. 7. MAGONJWA PAMOJA NA WADUDU WANAO ADHIRI MMEA. *Magonjwa. Zao hili hushambuliwa kwa kiasi kidogo na magonjwa kama 1;kuoza kwa mizizi 2;kunyauka kwa ncha ya jani *Wadudu. Wadudu wengi wanashambulia zao hili lakini hawasababishi madhara makubwa ,mfano konokono hula kiasi kidogo cha majani pamoja na kuku hushambulia mizizi. NB. Uvunaji wa zao la vanilla hufanyika kati ya mwezi wa 6 mpaka 9 kulingana na wakati wa ua lilipo chanua ,maharagwe yake huvunwa yanapokuwa yamekomaa na ncha yake kuwa na rangi ya unjano.Uvunaji hufanyika kwa kutumia kisu chenye ncha kali sana au mikono . Pia vanilla hunwa kabla ya kuiva na baada ya hapo huvundikwa kwa ajili ya kutengeneza kemikali inayojulikana kama vanillin,inayotoa harufu nzuri pamoja na ladha nzuri inapotumika katika kutengenezea vyakula pamoja na vinywaji

UFUGAJI WA KUKU PAMOJA NA MABANDA YAKE

monk MAANDALIZI YA KUPOKEA VIFARANGA Kabla ya kuleta vifaranga Maranyingi ufugaji wa kuku huanza na vifaranga, na kwa kuwa vifaranga huwe...