Load

Tuesday, October 23, 2018

UFUGAJI WA KUKU PAMOJA NA MABANDA YAKE

monk MAANDALIZI YA KUPOKEA VIFARANGA
Kabla ya kuleta vifaranga
Maranyingi ufugaji wa kuku huanza na vifaranga, na kwa kuwa vifaranga huweza kuathirika haraka na mazingira, maandalizi mazuri kabla hawajaletwa ni muhimu sana.

Vifaranga wakiwa na umri wa juma moja huhitaji eneo la sentimeta za mraba 65 kila mmoja au mete moja ya mraba kwa vifaranga 120 hadi 150.

Kabla hujaingiza vifaranga safisha banda lako vizuri ndani na nje pamoja na mazingira yake. Pakikauka paka chokaa kwenye kuta zote. Hakikisha banda limekuwa tupu kwa wiki moja au mbili baada ya kusafishwa. Tandaza maranda bandani kisha juu yake weka magazeti au "chick papers".

Hakikisha una idadi ya kutosha ya vyombo vya chakula na maji kulingana na idadi ya kuku. Pia uwe na chakula bora cha kuanzishia.

Tayarisha chanzo cha joto angalau kwa saa 3 - 5 kabla vifaranga havijaingia ili joto la nyuzi joto 33 - 35 lipatikane.

Ukishawaleta vifaranga
Hesabu na kukagua vifaranga wakati wa kuweka bandani. Changanya maji safi na "glucose" pamoja na dawa za kuanzishia kisha wapatie. Dawa hii wapatie kwa siku 3 hadi 5 kulingana na maelezo ya dawa utakayotumia. Wapatie chakula baada ya saa 2 - 3 toka walipowasili na kunywa maji yenye "glucose" na dawa za kuanzishia.

Tumia kitabu kutunza kumbukumbu ya idadi, tarehe, aina ya vifaranga na chakula, kampuni ya vifaranga, magonjwa na matibabu yake, madawa yaliyotumika na kinga, na vifo toka siku ya mwanzo hadi wakati wa kuuza.
NB.

Kuna aina mbali mbali za kuku
Kuku wa nyama(broiler)
Kuku Wa mayai(layers)
Kuku chotara(mayai-nyama)
Kuku wa kienyeji.
Mabanda na ujenzi wake
KUKU WA NYAMA
'''Kuku wa nyama''' ni aina ya kuku anayefugwa kwa ajili ya nyama .Kuku wa nyama wa kisasa wa biashara  huzalishwa kwa wingi, huwa na nyama fanisi na hukua kasi kuliko kuku wa mayai au kuku wanaotumika kwa zote mbili. Wanabainishwa kutokana na ukuaji haraka, uwiano kula ulio juu na viwango vya chini ya shughuli. Kuku wa nyama mara nyingi huwa tayari wafikia uzito wa kg1-1.5
Wana manyoya meupe na ngozi ya manjano. Kuku hawa wa faida katika nyama kwa sababu inakosa "nywele" za kawaida ambazo wengi wa aina tofauti wanabidi kuchomwa baada ya kutoa manyoya. Kuku wote wa kike na kume huchinjwa kwa ajiliya nyama zao. 
KUKU WA MAYAI
Hawa ni aina tu ya kuku wanaotaga na kutotoa pia vifaranga.Lakini kwa mfungaji anaweza kujiongeza zaidi kwa kuwa kununua incubator (kitotoresha mayai),kwa njia unawasaidia sana kuku wako kutopoteza nguvu na muda kuatamia mayai.
Pia kuku hawa wakilishwa vizuri aina ya vyakula kama
Majani ya mipapai
Leukaena(pia ni aina ya majani kama inavyo onekana katika picha) huongeza unjano katika kiini cha yai la kuku wa kisasa
Lakini pia ni muhimu kuku wa kutaga kupewa sehemu ya kutagia mayai yake (laying nest)kuepuka mayai kupata nyufa /mipasuko ambayo hupelekea mayai kukosa ubora katika soko.
KUKU CHOTARA
Ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara. Tunaposema chotara tuna maanisha ni mchanganyingo wa aina mbili za kuku. Mfano kuku wangu ni mchanganyiko wa kienyeji na kenbro wanajulikana kama kuku wa kenya. Sifa ya kuku chotara ni kama ifuatavyo,
 1. Wanastahimili sana magonjwa.
 2 Wanataga mayai mengi mpaka 240 kwa mwaka kama ukiwalisha vizuri kwa miaka mitano
 3. Wanakua haraka sana. Wanafikisha mpaka kilo 3 kwa muda wa miezi mitatu kama ukiwalisha vizuri
 4.Anatumika kama kuku wa nyama na mayai
 Ukitaka kufuga kuku kibiashara usimwachie kuku kuhatamia mayai kwani unampotezea muda wa kutaga. Kusanya mayai weka kwenye mashine ya kutotolea vifaranga. Ukitaka kupata faida kubwa usinunue chakula bali tengeneza mwenyewa kwani bei za vyakula zimepanda sana.
Tetea wa chotara hula kiasi cha 6.8kg kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 1.8kg kwa kipindi hicho.
Jogoo chotara huweza hula kiasi cha 6.8kg kwa muda wa miezi mitano na kuweza kufikia uzito wa 2.6 kwa muda huo.
Matetea chotara huanza kutaga ndani ya muda wa miezi mitano mpaka sita kutegemea na utunzaji na vyakula wanavyopewe.Ili kuku hawa watage sana wanatakiwa kula angalau 122g kwa siku za chakula kizuri ili kuweza kutaga kwa muda mrefu.
Kuku hawa wataanza tabia ya kudonoana kama wasipopewa chakula kizuri na chenye virutubisho vya kutosha pamoja na madini.Kuku hawa hudonoana sana na wakati mwingine hupelekea vifo na vidonda
KUKU WA KIENYEJI
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. Maelekezo yafuatayo yatatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.
Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.
2.  Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.
3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.
5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.
7.  Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.
  Magonjwa na kinga kwa kuku wote
Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.
Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.
Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.
Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.
Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.
Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo
Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.
SEHEM ZA BANDA BORA LA KUKU
Zifuatazo ni sehem za banda bora la kuku kulingana na aina ya kuku:-
1. Sehem za kutagia (kama ni kuku wa mayai au wa kienyeji).
Katika banda bora la kuku wanaotarajiwa kutaga inapaswa kuwepo na sehem za kutagia zijulikanazo kwa jina la viota. Viota vinaweza kutengenezwa kwa mtindo wa kuku mmoja mmoja au ushirika.
2. Sehem ya kutembelea.
          Ni ukumbi mkubwa kulingana na idadi ya kuku, ambao ndani yake kunakuwa na vyombo vya maji na chakula, pamoja na kuku wenyewe.
3. Sakafu
          Zipo aina mbalimbali za sakafu kama ifuatavyo:-
     a) Sakafu ya saruji
             Ni vema zaidi ukajenga sakafu ya saruji kisha ukaweka maranda juu yake ili kuzuia ubaridi
          unaotoka sakafuni, na vilevile kupata
wepesi wakati wa kufanya usafi.
      b) Sakafu ya udongo au mawe
              Jaza udongo wa mfinyanzi au mawe kisha siliba vizuri acha pakauke mwisho weka maranda
           kwa wingi.
      c) Sakafu ya chaga
Banda hujengwa kisha huwekwa chaga umbali wa futi mbili kutoka chini, chaga inaweza
          ikawa ya banzi, "chicken wire" au fito ili kuruhusu kinyesi cha kuku kudondoka choini.
4. Ukuta
          Unaweza kujenga ukuta kwa kutumia nguzo, pamoja na mabanzi au fito kisha kuzibwa vizuri na kuacha sehemu kubwa kwa ajili ya madirisha. Pia unaweza kutumia tofali za kuchoma, saruji au tofali za udongo kwa kujengea na kuacha sehem kubwa kwa ajili ya madirisha.
5. Paa
       Vifaa vya kuezekea vinaweza kuwa ni vigae, nyasi, makuti au bati.


UJENZI WA BANDA BORA LA KUKU 
         Mfugaji anaweza kudhani kuwa mradi wa kuku unaweza kumpatia faida kubwa bila kujali uwepo wa banda zuri na imara.
 Banda lililojengwa imara hudhibiti maadui wa kuku na kufanya uzalishaji kuwa bora zaidi.

Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa  ujenzi wa banda.
1. Idadi ya kuku
        Kabla ya kuanza kujenga banda, mfugaji anatakiwa kujua kuwa anataka kufuga kuku wa aina gani na wangapi. Hii itamwezesha mfugaji kujua ukubwa wa banda linalohitajika.

2. Uwezo wa mfugaji kifedha.           Ujenzi wa banda unahitaji fedha nyingi, hivyo ni lazima mfugaji ajue kuwa banda analotaka kujenga atalimaliza.

3. Eneo la kujenga banda.      Mfugaji lazima awe na eneo la kujenga banda na liwe na sifa zifuatazo:-
•Mwinuko - Iwe sehemu iliyoinuka isiyotuamisha maji kirahisi.
•Eneo lisiwe mbali na sehemu ya kuishi ili kuweza kulinda.
•Uwezekano wa upanuzi - Sehemu iwe pana na kubwa ili mradi ukiwa mkubwa iwepo sehemu ya upanuzi.
Sifa za banda bora la kuku.
 1. Liwe limejengwa mahali palipokingwa na upepo mkali kwa miti.
 2. Liwe na mwanga wa kutosha.
 3. Madirisha yaruhusu hewa safi kuingia na chafu kutoka (Cross Ventilation).
 4. Sakafu isiruhusu maji kutuama wala maeneo yanayozunguka banda.
 5. Paa lisiruhusu mvua kuingia.
 6. Banda liwe linasafishika kwa urahisi.
 7. Kuta ziwe imara na zizuie wanyama waharibifu kuingia.
 8. Banda liwe na nafasi ya kutosha kwa ajili ya kuku, vyombo vya maji na chakula, na mhudumu
     kupita.
NB.



Prepared by
Moses Joshua

Email 📧 mosesmugisha70@gmail.com
Phone 📱 0766260178
       0687849821
Qualification. Animal health and production(certificate & Diploma level 6)

Saturday, October 20, 2018

ZIJUE AINA KUU MBILI ZA NGURUWE KWA FAIDA YA UFUGAJI.

Nguruwe ni mnyama ambaye katika uhalisiwa wa ukuaji wake anakua ndani ya muda mfupi kumlinganisha na ng'ombe .Katika utafiti wa muda mwingi kwa miaka kadhaa iliyopita inaonesha nguruwe ni mnyama anayekuwa ndani ya miezi mitatu na ndani ya muda huo akawa na uwezo wa kupanda/kupandwa .


Nguruwe pia ni mnyama mwenye uwezo wa kuzaa watoto wengi kwa uzao mmoja,Ana uwezo wa kuzaa watoto kuanzia saba(7)-kumi na mbili(12).


Pia nguruwe wanauwezo tofauti wa kuchunga na kulea watoto wao mpaka kufikia kipindi cha watoto wao kukua na kuwa na uwezo pia wa kuzaa na kuzalisha pia .


Pia nguruwe ni mnyama mzuri ambaye anaongezeka kilo zake kulingana na matunzo na aina ya vyakula anavyopewa na mhudumu anaye muhudumia,Pia jambo hili linakuwa ni jema sana kwa mtu anaye tazamia kufuga au ambaye tayali yupo katika ufugaji akitarajia kufanya biashara ya kuuza nyama ya nguruwe kulingana na soko lake linavyo taka.


AINA MBILI KUU NA NZULI ZA NGURUWE KWA UZALISHAJI NA BIASHARA.


Hizi ni aina mbili za nguruwe wa kisasa ambao asili yake inatokana na nchi za nje
a.landrace
-Hawa ni nguruwe wenye miili mirefu wasikio yake yameshuka kwa kufunikiza uso wake
-Wanauwezo wa kuzaa watoto wengi kwa uzao mmoja .
-Hawana uwezo mkubwa wa utunzaji wa watoto ,kwa mfugaji aina hii ya nguruwe ni nzuri zaidi kwa ajili ya uzalishaji wa nyama kwa ajili ya kufanya biashara.


b.large white
-Hawa ni nguruwe ambao sio ware sana bali wana kimo cha kati
-Masikio yao yamesimama
-Anauwezo mkubwa wa kuzaa watoto wengi na kuwatunza watoto wake
-Ni wapole pia ni nguruwe wanao ongezeka kilo zao ndani ya muda mfupi kulingana na matunzo yao.



FAIDA ZA KUKU WA KISASA KWA BIASHARA

UTANGULIZI.
kuku wa kisasa (broiler) ni mbegu ya kuku iloyoboreshwa kitaalam zaid katika maabala kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watumiaji ndani ya muda mfupi.


MAHITAJI.
kwa mtu anaye tarajia kuwa mfugaji wa kuku wa kisasa lazima atambue baadhi ya mahitaji kwa ajili ya kuendeleza mpango kazi wake.


A.Eneo kwa ajili ya kujenga banda.
Angalau eneo lake liwe na ukubwa wa kutosha kwa ajili kujenga banda.


B.Zana na mahitaji ya kujengea
Yawe yenye kupatikana katika eneo husika kuepuka ongezeko la gharama za kufanyia manunuzi ya mahitajo hayo.


C.Aina ya kuku kulingana na mahitaji ya mfugaji.
Mfugaji lazima ajue ni aina gani ya kuku anaotamani kuwa fuga na soko lake kwa ujumla.


D.Upatikanaji wa vyakula,matibabu kwa ajili ya mifugo.
Pia mkulima lazima ajue kuwepo na upatikanaji wa mahitaji kwa ajili ya kuku wake kama vykula tofauti tofauti,madawa kwa ajili ya matibabu kuepukana na vifo visivyo vya lazima katika banda lake.


NB.
Ni kuku wenye uwezo wa kuku kwa uharaka zaidi kuanzia wiki nne hadi sita na kuweza kukidhi mahitaji ya watumiaji.
Pia ukuaji wake unategemea na matunzo katika
A.Vyakula
B.Matibabu
C.Mazingira kwa ujumla(miundo mbinu ya mabanda na usafi).
Pia kwa mfugaji au kwa mtu anayependa kuwa mfugaji wa kuku hawa wa kisasa ni lazima afahamu kuwa baridi sio rafiki kabisa wa kuku wa kisasa hasa wakiwa katika hatua ya vifaranga.

UFUGAJI WA KUKU PAMOJA NA MABANDA YAKE

monk MAANDALIZI YA KUPOKEA VIFARANGA Kabla ya kuleta vifaranga Maranyingi ufugaji wa kuku huanza na vifaranga, na kwa kuwa vifaranga huwe...