Nguruwe ni mnyama ambaye katika uhalisiwa wa ukuaji wake anakua ndani ya muda mfupi kumlinganisha na ng'ombe .Katika utafiti wa muda mwingi kwa miaka kadhaa iliyopita inaonesha nguruwe ni mnyama anayekuwa ndani ya miezi mitatu na ndani ya muda huo akawa na uwezo wa kupanda/kupandwa .
Nguruwe pia ni mnyama mwenye uwezo wa kuzaa watoto wengi kwa uzao mmoja,Ana uwezo wa kuzaa watoto kuanzia saba(7)-kumi na mbili(12).
Pia nguruwe wanauwezo tofauti wa kuchunga na kulea watoto wao mpaka kufikia kipindi cha watoto wao kukua na kuwa na uwezo pia wa kuzaa na kuzalisha pia .
Pia nguruwe ni mnyama mzuri ambaye anaongezeka kilo zake kulingana na matunzo na aina ya vyakula anavyopewa na mhudumu anaye muhudumia,Pia jambo hili linakuwa ni jema sana kwa mtu anaye tazamia kufuga au ambaye tayali yupo katika ufugaji akitarajia kufanya biashara ya kuuza nyama ya nguruwe kulingana na soko lake linavyo taka.
AINA MBILI KUU NA NZULI ZA NGURUWE KWA UZALISHAJI NA BIASHARA.
Hizi ni aina mbili za nguruwe wa kisasa ambao asili yake inatokana na nchi za nje
a.landrace
-Hawa ni nguruwe wenye miili mirefu wasikio yake yameshuka kwa kufunikiza uso wake
-Wanauwezo wa kuzaa watoto wengi kwa uzao mmoja .
-Hawana uwezo mkubwa wa utunzaji wa watoto ,kwa mfugaji aina hii ya nguruwe ni nzuri zaidi kwa ajili ya uzalishaji wa nyama kwa ajili ya kufanya biashara.
b.large white
-Hawa ni nguruwe ambao sio ware sana bali wana kimo cha kati
-Masikio yao yamesimama
-Anauwezo mkubwa wa kuzaa watoto wengi na kuwatunza watoto wake
-Ni wapole pia ni nguruwe wanao ongezeka kilo zao ndani ya muda mfupi kulingana na matunzo yao.
ggh
Blog Archive
Search This Blog
About Me
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
UFUGAJI WA KUKU PAMOJA NA MABANDA YAKE
monk MAANDALIZI YA KUPOKEA VIFARANGA Kabla ya kuleta vifaranga Maranyingi ufugaji wa kuku huanza na vifaranga, na kwa kuwa vifaranga huwe...
-
1.zao la vanila asili yake ni Amerika ya kati huko mexico,costa rica pamoja na guatemala ambako lilianza kutumika katika karne ya 15 na kufi...
-
monk MAANDALIZI YA KUPOKEA VIFARANGA Kabla ya kuleta vifaranga Maranyingi ufugaji wa kuku huanza na vifaranga, na kwa kuwa vifaranga huwe...
-
Nguruwe ni mnyama ambaye katika uhalisiwa wa ukuaji wake anakua ndani ya muda mfupi kumlinganisha na ng'ombe .Katika utafiti wa muda mwi...
1xbet korean ✔️ 100% Bonus Offers - legalbet.co.kr
ReplyDelete1xbet is a betting website that offers a variety of worrione sports, such as football, basketball, 바카라 사이트 rugby, 1xbet korean soccer and other games.